Na Joseph Ngilisho,Arusha
Watu wawili wakazi wa Wilayani Arumeru Mkoani Arusha,Christophe Malicki{61} na Kelvin Richard{24} wamefungwa kifungo cha maisha jela katika matukio mawili tofauti ya kubaka na kulawiti.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru,Itikija Nguvava alisema kuwa Katika tukio la kwanza la kubaka linamhusu mzee Malicki Mkulima Mkazi wa Kijiji cha Imbaseli kata ya Leguliki Wilayani Arumeru alitenda kosa hilo march 4 mwaka huu kijijini hapo baada ya kumbaka mtoto wa kike wa miaka 8 aliyekuwa akichunga mbuzi.
Hakimu Nguvava alisema katika hukumu yake kuwa amejiridhisha pasipokuwa na shaka yoyote kwa mzee Malicki alitenda kosa hilo baada ya kujiridhisha na kielelezo cha hati ya matibabu PF3.
Alisema mbali ya hilo pia amejilithisha na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri waliotoa ushahidi wao mahakamani na utetezi uliotolewa na mhanga haukuwa na nguvu ya kumwonoa katika shitaka hilo.
Baada ya kumtia hatiani Mhanga alipewa nafasi ya kujitetea na mzee Malicki alisema kuwa yeye ni Mzee na anafamilia kubwa inayowategemea na kosa hilo ni kosa lake la kwanza kwani sheteni alimpitia na kujikuta akifanya ubaka hivyo aliomba mahakama impunguzie adhabu.
Jopo la Waendesha Mashitaka wa Serikali likiongozwa na Grace Medikenya lilimwambia Hakimu Nguvava Kutoa adhabu kali kwa mzee Malicki kwani tabia ya kubaka wilayani Arumeru Mkoani Arusha imekithili ili iwe fundisho kwa wengine.
Hata hivyo utetezi huo haukumsaidia kwani Hakimu Nguvava alimfunga Kifungo cha maisha Mzee Malicki na kutoa onyo kwa wazee wengine wenye tabia hiyo kuacha mara moja.
Katika hukumu nyingine ya kulawiti Richard mkazi wa Kijiji cha Kambi ya Pili kata ya Imbaseli Arumeru alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti chooni mtoto wa kike wa miaka 8 katika tukio lililotokea Kijijini hapo aprill 27 mwaka huu.
Akisoma hukumu,Hakimu Mkazi wa Wilaya Arumeru Mkoani Arusha ,Mwamini Kazema alisema kuwa amemfunga kifungo cha maisha Richard baada ya kulidhika na ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri na ushahidi wa kielelezo kimoja cha PF3.
Hakimu Kazema alisema utetezi wa mtuhumiwa na mashahidi wake wawili bado haukuwa na nguvu za kuthibitisha kuwa yeye hakutenda kosa hilo kwani hawakuwa na kielelezo chochote cha ushahidi kuthibitisha hilo hivyo nakutia hatiani kwa kosa hilo.
Baada ya kutiwa hatiani Mtuhumiwa alipewa nafasi ya kujitetea na mtuhumiwa kudai kuwa yeye bado ni kijana anayeanza maisha na kosa hilo lilikuwa la kwanza na tamaa ya ngono ilimfikisha hapo na aliomba kusamehewa au kupewa adhabu ndogo kwani ni mara yake ya kwanza kwake kutenda kosa hilo.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali,Grace Medikenya yeye alimwomba Hakimu kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kwani vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto wadogo wa kike vimekuwa vingi katika wilaya ya Arumeru ili iwe fundishi kwa wengine.
Baada ya hoja ya hiyo Hakimu alisema na kumwambia mtuhumiwa kuwa anamfunga kifungo cha maisha baada kulidhika na ushahidi wa jamhuri na kielelezo kilichotolewa mahakamani hapo ili iwe fundisho kwa wengine
.....Ends......
0 Comments