Ad
Breaking🔥

LISSU AACHIWA HURU KESI YA UHaini, AHUKUMIWA KWA UCHOCHEZI

LISSU AACHIWA HURU KESI YA UHaini, AHUKUMIWA KWA UCHOCHEZI

Na Joseph Ngilisho | DAR ES SALAAM

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemuondolea Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, hatia ya uhaini, lakini imemhukumu kwa kosa la uchochezi baada ya kubaini kuwa shtaka hilo limethibitishwa na upande wa Jamhuri.

Hukumu hiyo imesomwa leo, Ijumaa, Novemba 6, 2026, na Jaji Dunstan Ndunguru, aliyekuwa akiongoza jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo.

Katika uamuzi wake, mahakama imesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kuwa Lissu alikuwa na nia ya kuitishia Serikali kupitia kauli zake, jambo lililokuwa msingi wa shtaka la uhaini.

Hata hivyo, mahakama imeridhika kuwa ushahidi uliowasilishwa umeweza kuthibitisha kosa la uchochezi, hivyo kumtia hatiani Lissu kwa kosa hilo kama mbadala wa shtaka la uhaini.

Akifafanua msingi wa kisheria wa uamuzi huo, Jaji Ndunguru alisema Kifungu cha 319 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinaipa mahakama mamlaka ya kumtia mshtakiwa hatiani kwa kosa dogo lililothibitishwa, hata kama kosa hilo halikuwa miongoni mwa mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yake.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Lissu ametiwa hatiani kwa kosa la uchochezi chini ya Kifungu cha 390 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa Lissu ameondolewa katika shtaka kubwa la uhaini, lakini bado anakabiliwa na hatia ya uchochezi.

Ends

Post a Comment

Previous Post Next Post