ABIRIA ZAIDI YA 40 WAPONUSHA KIFO, Basi la Abood LATEKETEA KWA MOTO ISAKA
..Hakuna aliyepoteza maisha, chanzo cha moto bado kuchunguzwa
By Arushadigital|KAHAMA
BASI la kampuni ya usafirishaji ya Abood lililokuwa na zaidi ya abiria 40 likiteketea kwa moto katika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, huku abiria wote wakinusurika kifo.Basi hilo lenye namba za usajili T285 EAV lilikuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kagera, kabla ya kukumbwa na tukio hilo wakati likiwa safarini.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, SSP Stanley Luhwago, alisema kikosi chake kilifika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima moto huo.
Ends
إرسال تعليق