Ad
Breaking🔥

MKUU WA MKOA ATUMBULIWA, SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MPYA WA VIONGOZI, ANGELINE MABULA ATEULIWA MKUU WA MKOA WA TABORA

Na Joseph Ngilisho | ARUSHA DIGITAL

DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wapya watatu, akiwemo Angeline Lubala Mabula aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 28, 2026, na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Shaaban Kissu, Mabula anachukua nafasi ya Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Katika uteuzi huo, Rais Samia pia amemteua Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kabla ya uteuzi huo, Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu ambaye amemaliza muda wake.

Aidha, Rais Samia amemteua Omar Ali Omar kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kabla ya uteuzi huo, Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Zanzibar.

Omar anachukua nafasi ya Mohamed Khamis Hamad ambaye amemaliza muda wake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uapisho wa viongozi hao utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Uteuzi huo ni sehemu ya mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Rais Samia katika nafasi za utumishi wa umma na taasisi za kitaifa.

Chanzo: Taarifa ya Ikulu, Oktoba 28, 2026.

Post a Comment

أحدث أقدم