Ad
Breaking🔥

DIWANI WA CCM ADAIWA KUPIGWA SHOKA NA KUFARIKI DUNIA

DIWANI WA CCM ADAIWA KUPIGWA  SHOKA NA KUFARIKI DUNIA

Mauaji yahusishwa na mapigano ya wakulima na wafugaji

Na Arushadigital | TUNDURU

DIWANI wa Kata ya Misechela, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Zuberi, anadaiwa kuuawa kwa kushambuliwa kwa shoka katika mapigano yanayodaiwa kuwa baina ya wakulima na wafugaji.

Tukio hilo linaongeza wasiwasi kuhusu usalama wa wananchi wa wilaya hiyo, ambayo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita imeripotiwa kukumbwa na mfululizo wa mapigano baina ya makundi hayo.

Mapigano hayo yamedaiwa kusababisha vifo, majeruhi, ulemavu, uharibifu wa mali na miundombinu ya umma.

Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu mazingira ya tukio la kuuawa kwa diwani huyo, waliohusika na hatua zilizochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama hazijaelezwa katika taarifa zilizopatikana.

Ends..

Post a Comment

أحدث أقدم