DC ARUMERU KUANZISHA MFUMO WA KUPOKEA KERO ZA WANANCHI
Na Joseph Ngilisho | ARUMERU
MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, ameanzisha utaratibu wa ChapKwaDCArumeru kwa lengo la kupokea na kutatua kero za wananchi moja kwa moja.
Kupitia mfumo huo, wananchi wanatakiwa kutuma kero zao kwa SMS au WhatsApp kupitia namba 0744 663 739, huku akiahidi kufuatilia na kutoa mrejesho ndani ya siku saba.
Lugangira amewataka wananchi kueleza majina yao, maeneo wanayoishi, kero zinazowakabili, muda zilipoanza na hatua walizochukua, ili kurahisisha ufuatiliaji na kuharakisha utatuzi wake.Ends

إرسال تعليق