Ad
Breaking🔥

LUKUMAY AILILIA FAMILIA YA AMINIEL MOLLEL,AWAFARIJI KWA KUITEMBELEA KUWAPA TABASAMU

LUKUMAY AWAFARIJI WAFIWA NA KIONGOZI WA OLOIRIEN

Na Joseph Ngilisho | ARUMERU

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lembulung Lukumay, amewatembelea na kuwapa pole mjane na watoto wa marehemu John Aminieli Mollel, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Oloirien, kufuatia kifo cha mpendwa wao.

Katika ziara hiyo, Dkt. Lukumay amewafariji wafiwa na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape nguvu, uvumilivu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo.

Mbunge huyo amesisitiza umuhimu wa kuwa karibu na familia iliyopata msiba, akiwapa pole mjane, watoto na ndugu wa marehemu kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Lukumay amewaombea wafiwa waendelee kuwa na moyo wa subira na kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki cha majonzi

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم