LUKUMAY AMLILIA MUME WA RAIS SAMIA
Na Joseph Ngilisho | ZANZIBAR
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lembulung Lukumay, ni miongoni mwa watu mashuhuri walioungana na Watanzania na viongozi mbalimbali kumlilia na kutoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mumewe, Mheshimiwa Hafidh Ameir Hassan.Dkt. Lukumay amefikisha salamu zake za pole kwa Rais Samia na familia yake, ikiwa ni sehemu ya viongozi walioungana na Rais katika kipindi hiki cha majonzi.
Septemba 8, 2026, Dkt. Lukumay alikwenda katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui, Zanzibar, ambako alisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Hafidh Ameir Hassan.
Aidha, Dkt. Lukumay alikwenda nyumbani kwa Rais Samia, Kizimkazi, Zanzibar, na kuungana na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliokwenda kumfariji Rais pamoja na familia yake.
Katika tukio hilo, Dkt. Lukumay alitoa pole kwa Rais Samia, akimtakia nguvu na subira katika kipindi hicho kigumu cha msiba wa mumewe.
Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, huku taarifa za kifo chake zikitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi.
Ends
إرسال تعليق