KITENDO CHA UNYANYASAJI WA KINGONO KWA MTOTO CHAIBUA HUKUMU YA MIAKA 20 JELA
By Arushadigital-TABORA.
Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama baada ya shauri lililokuwa likimkabili Kitundu kusikilizwa na upande wa mashtaka kuwasilisha ushahidi uliowezesha Mahakama kumtia hatiani.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Twaha Lulengelule, amesema Kitundu amehukumiwa kifungo hicho baada ya Mahakama kuthibitisha kosa alilokuwa akikabili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, tukio hilo lilitokea Machi 22, 2026, ambapo Kitundu anadaiwa kumchukua mtoto huyo na kwenda naye katika kibanda cha filamu kilichopo Mtaa wa Nyerere, ambako alifanya kitendo cha unyanyasaji wa kingono dhidi yake.
Baada ya kukamilika kwa mchakato wa kisheria na shauri hilo kusikilizwa, Mahakama ilimtia hatiani Kitundu na kumhukumu kutumikia kifungo cha miaka 20 jela.
Jeshi la Polisi limeendelea kuhimiza jamii kutoa taarifa mapema kuhusu vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto, ili hatua za kisheria zichukuliwe na kulinda usalama na haki za watoto.
Ends

Post a Comment