Ad
Breaking🔥

BASATA YAMFUNGIA MZIKI HARMONIZE

BASATA YAMFUNGIA HARMONIZE

By Arushadigital Dar es Salaam. 

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewafungia msanii Harmonize na muongozaji wa video Director Kenny kujihusisha na shughuli za sanaa hadi watakapotekeleza maamuzi yaliyotolewa na Baraza hilo kufuatia ukiukwaji wa maadili kupitia video ya wimbo KUDOS.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya BASATA kubaini ukiukwaji wa maadili katika video hiyo, ambayo ni miongoni mwa kazi zilizopo kwenye albamu mpya ya Harmonize inayojulikana kwa jina la 31.

Katika maamuzi yake, BASATA imewataka Harmonize na Director Kenny, kila mmoja kulipa faini ya Sh5 milioni, pamoja na kuiondoa video hiyo kwenye mitandao yote ya kijamii.

BASATA pia imeeleza kuwa kufungiwa kwao kuendelea na shughuli za sanaa kutadumu hadi watakapotekeleza masharti hayo yaliyotolewa na Baraza.

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo video na maudhui ya wasanii kwenye mitandao ya kijamii yakiendelea kuwa sehemu kubwa ya tasnia ya burudani, huku mamlaka za sanaa zikisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili na kanuni zinazosimamia kazi za wasanii nchini.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم