Ad
Breaking🔥

DR. DANIEL LEMA, MWANZILISHI WA REDIO SAFINA ARUSHA AFARIKI DUNIA

DR. DANIEL LEMA, MWANZILISHI WA REDIO SAFINA ARUSHA AFARIKI DUNIA

Na Joseph Ngilisho| Arusha

MWANZILISHI wa Huduma ya Redio Safina Arusha, Dkt. Daniel Lema, amefariki dunia, huku familia yake ikieleza kuwa ameacha alama kubwa kupitia huduma hiyo na katika maisha ya watu aliowahudumia.

Dkt. Lema amefariki dunia Jumatano, Septemba 23, 2026, katika Hospitali ya Selian (ALMC) jijini Arusha, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.




Taarifa ya kifo hicho imetolewa na mke wa marehemu, Mama Hellen Daniel Lema, ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma ya Safina Redio Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia, maandalizi ya mazishi yanaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Kaloleni, jijini Arusha, huku ratiba rasmi ya mazishi ikitarajiwa kutangazwa baada ya kukamilika kwa taratibu zinazohusiana na msiba huo.

Familia imesema kifo cha Dkt. Lema ni pigo kwa familia, Huduma ya Redio Safina, waumini, wafanyakazi, wasikilizaji pamoja na watu wengine walioguswa na huduma yake kwa kipindi cha uhai wake.

Katika taarifa hiyo, familia imesema marehemu alijitoa kwa moyo wake wote kulitumikia kusudi la Mungu kupitia Huduma ya Redio Safina, akieleza kuwa ameacha alama katika maisha ya watu wengi.

“Alijitoa kwa moyo wake wote kulitumikia kusudi la Mungu kupitia Huduma ya Redio Safina na ameacha alama katika maisha ya watu wengi,” imeeleza taarifa ya familia.

Kifo cha Dkt. Lema kimeacha pengo katika Huduma ya Redio Safina, ambayo imekuwa sehemu ya shughuli za uinjilisti na mawasiliano ya kidini jijini Arusha.

Familia imewataka wafanyakazi wa Huduma ya Redio Safina, ndugu, jamaa, marafiki, waumini na wasikilizaji wa redio hiyo kuendelea kuwa pamoja na familia na kumpa pole Mama Hellen Daniel Lema pamoja na wanafamilia katika kipindi hiki cha majonzi.

Ratiba ya mazishi na taarifa nyingine kuhusu taratibu za kuaga mwili wa marehemu zinatarajiwa kutolewa na familia baada ya kukamilika kwa maandalizi.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم