Breaking🔥

NABII TITO YAMKUTA AKAMATWA DAR KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

NABII TITO AKAMATWA DAR KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

By Arushadigital

DAR ES SALAAM. Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imemtia mbaroni Tito Onesmo Machibya, maarufu kama “Nabii Tito,” kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo, kutumia lugha ya matusi na kufanya uchochezi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, tukio hilo limetokea Agosti 15, 2026, saa 10:20 jioni, katika eneo la Sinza Makaburini, Ubungo, Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Tito, ambaye ni mkazi wa Buza Sigara, Temeke, amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, polisi wanaendelea kukamilisha taratibu za kisheria kabla ya kumfikisha katika mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza kwa kina aina ya taarifa zinazodaiwa kuwa za uongo, matusi yaliyodaiwa kutolewa wala namna vitendo hivyo vinavyodaiwa kuwa na uchochezi.

Post a Comment

أحدث أقدم