NOEL SEVERE AWASHUKURU WALIOSHIRIKI MAZISHI YA ANNA SEVERE
Na Joseph Ngilisho- ARUMERU
Akizungumza kwa niaba ya familia mara baada ya mazishi hayo, Noel ambaye pia ni Mwanafamilia alisema ushiriki mkubwa wa viongozi na wananchi katika kipindi chote cha msiba umeipa familia faraja na nguvu ya kukabiliana na majonzi ya kumpoteza mpendwa wao.
Aliwashukuru viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma na ngazi mbalimbali, viongozi wa Serikali, taasisi mbalimbali, viongozi wa dini, pamoja na wananchi wote waliofika kutoa pole na kushiriki shughuli za mazishi.
Noel pia aliipongeza Kamati ya Mazishi kwa kazi kubwa iliyofanya kuanzia maandalizi hadi kukamilika kwa shughuli zote za mazishi, akisema familia haina cha kuwalipa wote waliojitolea zaidi ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awabariki.
"Kwa niaba ya familia, tunatoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliyesimama nasi katika kipindi hiki kigumu. Upendo na mshikamano mlioonyesha umetupa faraja kubwa. Mwenyezi Mungu awabariki na awalipe kwa wema wenu," alisema.
Aidha, alieleza kuwa familia itaendelea na ratiba zake za kifamilia kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kukamilika kwa shughuli za mazishi.
Mazishi ya Anna Severe yalihitimishwa kwa mamia ya waombolezaji kushiriki kutoa heshima za mwisho, huku familia ikisisitiza kuwa itaendelea kuuenzi upendo na mshikamano ulioonyeshwa na jamii wakati wote wa msiba.
Ends..













إرسال تعليق