SAMIA ATEUA KAMISHNA MPYA WA TANAPA
By Arushadigital
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Massana Gibril Mwishawa kuwa Kamishna mpya wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), akichukua nafasi ya Musa Nassoro Kuji ambaye amestaafu baada ya kumaliza muda wake wa Nyongeza wa utumishi.
Kabla ya uteuzi huo, Mwishawa alikuwa akihudumu kama Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Maendeleo ya Biashara ndani ya TANAPA, ambapo alishiriki kusimamia mikakati ya kuimarisha uhifadhi na kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika uchumi wa taifa.
Uteuzi huo unatarajiwa kuimarisha uongozi wa TANAPA katika kuendeleza uhifadhi wa rasilimali za taifa, kukuza utalii na kuongeza mapato yatokanayo na sekta hiyo muhimu ya uchumi.
Ends..

إرسال تعليق