MBUNGE LUKUMAY APOKEA UGENI MZITO BUNGENI KUTOKA OLJORO- ARUMERU

 LUKUMAY APOKEA UGENI MZITO BUNGENI KUTOKA OLJORO -ARUMERU MAGHARIBI 

Na Joseph Ngilisho|Arushadigital | DODOMA

Mbunge wa Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lembulung Lukumay, leo Juni 3, 2026, amepokea ugeni wa viongozi na wawakilishi wa wananchi kutoka Kata ya Oljoro waliomtembelea katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.


Ugeni huo ulijumuisha viongozi mbalimbali kutoka Kijiji cha Mbuyuni na maeneo ya Oljoro, akiwemo Diwani wa Kata ya Oljoro, Charles Miseyeki, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuyuni, Lembris Karani, Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Olmulo, Leskari Ole Rangai, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Endevesi, Peter Jeremiah Laizer, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mitong’wa, Muran Tajiri Molle, pamoja na wawakilishi wa wanawake Elizabeth Emmanuel kutoka Endevesi na Nataaendito Nguku kutoka Mitong’wa.

Akizungumza baada ya kuwapokea viongozi hao, Dkt. Lukumay alisema ziara hiyo ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya viongozi wa ngazi za msingi na mwakilishi wao bungeni katika kusukuma mbele agenda za maendeleo ya wananchi wa Arumeru Magharibi.


Alisema viongozi hao wamepata fursa ya kujionea shughuli za Bunge na kujadiliana naye kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu wananchi wa Kata ya Oljoro, ikiwemo huduma za maji, miundombinu na ustawi wa jamii.


Ziara hiyo imeelezwa kuwa hatua muhimu ya kuimarisha mahusiano kati ya wananchi, viongozi wa maeneo yao na taasisi za maamuzi za kitaifa, huku ikitoa nafasi ya kufikisha moja kwa moja changamoto na vipaumbele vya maendeleo vya Kata ya Oljoro kwa ngazi ya Bunge.

**Ends**

Post a Comment

أحدث أقدم