ASKOFU MKUU RUGAMBWA AFARIKI ITALIA

By Arushadigital 


Aliyekuwa Balozi wa Baba Mtakatifu nchi mbalimbali duniani Mtanzania Askofu Mkuu Novatus Rugambwa amefariki dunia usiku wa Septemba 16, 2025 huko Roma nchini Italia.


Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa Oktoba 08, 1957 mkoani Kagera nchini Tanzania, aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Upadre Julai 06, 1986 na Mhashamu Nestorius Timanywa, aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Machi 18, 2010, aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Uaskofu na Askofu Mkuu Tarcisio Pietro Evasio Kardinal Bertone, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican.


Amehudumu katika nchi mbalimbali kwa nafasi ya Balozi wa Baba Mtakatifu nchi hizo ni kama vile Angola, Honduras, Visiwa vya Fiji na kwingineko.


Post a Comment

0 Comments