TAKUKURU YAWANASA WATIA NIA 11 WA CCM,MCHAKATO WA TUHUMA ZAO UNAENDELEA

By arushadigtal 


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewahoji watia nia 11 wa nafasi ya ubunge katika Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia malalamiko ya rushwa yaliyowasilishwa dhidi yao.


Akizungumza katika semina maalum ya mapambano dhidi ya rushwa iliyofanyika Mjini Moshi 15 Julai 2025, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro, Mussa Chaulo, alisema malalamiko hayo yako katika hatua ya uchakataji ili kubaini iwapo yana ukweli.


Amesema  kuwa hadi sasa malalamiko 11 yameanza kufanyiwa kazi, na TAKUKURU inatarajia kukamilisha uchakataji wake kabla ya uteuzi rasmi wa wagombea.

Post a Comment

0 Comments