Na Joseph Ngilisho- ARUSHA
HATIMAYE Vita ya Kisiasa kati ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda na Mbunge wa Sasa wa jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo imekuwa rasmi mara baada ya Makonda kuchukua Fomu kwa lengo la kumng'oa Gambo katika jimbo hilo.
Makonda alikabidhiwa fomu mchana wa leo, Juni 28, 2025, na Katibu wa CCM, Wilaya ya Arusha, Timothy Sanga.
Mei 20, 2025, Makonda aliboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kwa kujiandikisha upya kwenye Kituo cha Hospitali ya AICC, Mtaa wa Mahakama, Kata ya Sekei, Jijini Arusha.
Juni 23, 2025, Rais Samia alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na Makonda hakuwapo katika uteuzi huo, jambo ambalo liliashiria anajitosa katika kinyang’anyiro hicho.
Kutokana na hatua ya Makonda kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho ni rasmi kwamba Makonda analitaka jimbo hilo kwa udi na uvumba kiasi kwamba kila mmoja anahitaji nguvu ya ziadi kushawishi wajumbe.
0 Comments