Na Joseph Ngilisho- ARUMERU
KATIBU MKUU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati jijini Arusha,JOHN TANAKI amejitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Arumeru Magharibi na kueleza azima yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo iwapo atapata uteuzi ndani ya Chama Chake.
Akiongea Mara baada ya kukabiliwa Fomu na katibu wa ccm wilaya ya Arumeru mapema leo juni 28,2025, Camilla Kigosi katika zoezi lililofunguliwa leo,Tanaki ambaye ni Msomi wa Chuo Kikuu alisema lengo la kujitosa kwenye nafasi hiyo ni kutumia haki yake ya msingi , kuwatumikia wananchi wa Arumeru Magharibi huku akiomba ridhaa ya uteuzi kupitia chama chake cha Mapinduzi CCM.
"Leo tarehe 28,Juni,2025 nimefika ofisi za chama chetu kuchukua fomu kutia nia nafasi ya ubunge,na kinachonisukuma ni kuwatumikia wananchi wa jimbo la Arumeru Magharibi na ninandoto ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama"
Alisema iwapo atateuliwa kugombea jimbo la Arumeru Magharibi aliahidi kutumika vema katika jimbo hilo na kuwahakikishia wananchi kutojutia uamuzi wao.
Mwingine aliyechukua Fomu Ni Hendri MEJOOR alisema lengo la kuchukua fomu ni kutaka kutoa mchango wake kuwatumikia wananchi katika maendeleo ya jamii.
MEJOOR ambaye alikuwa wa kwanza kuchukua Fomu katika ofisi hiyo,alisema leo ni mara ya tatu kujitosha kuwania uteuzi nafasi hiyo lakini bahati haikuwa yake kutokana na jina lake kutorudi ila kwa sasa anaamini jina lake litarejea na tapata uteuzi wa kupeperusha vema bendera kuwania jimbo hilo kwa sababu anaimani na chama chake.
Kwa upande wake Mbunge mtetezi wa jimbo hilo,Noar Lembris ambaye alikuwa wa pili kukabidhiwa fomu,alisema yapo mengi aliyoyafanya katika jimbo hilo la Arumeru Magharibi ila ameamua kurejea kuchukua fomu ili kutetea nafasi yake kwa nia ya kukamilisha baadhi ya miradi ya maendeleo .
Alisema ametekeleza vema ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kuwasemea wananchi wa jimbo hilo na kuifanya serikali kutekeleza vema maendeleo katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari .
Alisema kuna baadhi ya mambo hayajafanyika katika jimbo hilo na dhamira yake ni kuhakikisha maeneo yote yenye changamoto ya maji ,Madaraja ,Vivuko na Miundombinu ya barabara anakwenda kuikamilisha.
Ends....
0 Comments