MTIFUANO MKALI MIAMBA 10 IKICHUKUA FOMU UBUNGE ARUMERU MAGHARIBI KANALI WA JESHI, MHASIBU NGUNGAT NA MWALIMU EZEKIEL WAJITOSA KUMNG'OA LEMBRIS NOAR

 Na Joseph Ngilisho- ARUMERU 


CPA JULIUS PAUL NGUNGAT ni Miongoni mwa watia nia 10 waliojitokeza kuchukua Fomu ya ubunge katika jimbo la Arumeru Magharibi na hivyo kukoleza Joto la Uchaguzi jimboni humo.






Wengine waliochukua Fomu ni pamoja na Mwenyekiti wa ccm wilaya hiyo NOEL Emmanueli Severe,John Langidare Tanaki, HENDRI Obed Mejool,Johannes Lukumay,Amos Amon Kinyunyu,Elius Remmy Siana, Luteni Kanali Joel Paul Meidimi na Mwl Ezekiel Elphas Mollel .

Akiongea Mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na katibu wa ccm wilaya hiyo, Camilla Kigosi,Ngungat alisema ametumia haki yake ya msingi kuchukua fomu na anandoto ya kuwa mbunge wa jimbo hilo kuwakilisha wananchi iwapo tu chama chake kitampa ridhaa hiyo.

Naye Luteni kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi JWTZ,Joel Meidimi alisema kilichomsukuma kuchukua fomu ni kutaka kutoa mchango wake kuwatumikia wananchi wa jimbo lake.

"Mimi tageti yangu kubwa baada ya kustaafu utumishi wangu wa umma ni kuja kuungana na wananchi wangu kusaidia Taifa langu kuwatumikia wananchi kupitia nafasi ya ubunge"

Alisema ameamua kuja kumsaidia Rais Samia Suluhu Hasani katika jimbo hilo ili kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi.



Naye mwalim Ezekiel Elphas Mollel baada ya kukabidhiwa fomu alisema amewiwa kugombea nafasi hiyo kama haki ya msingi ya kila mwanachana na kuahidi kufanya mabadiliko katika jimbo hilo kuondoa changamoto zilizopo 

Mollel ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa ccm Taifa kutoka Arumeru Magharibi,alisema amejipanga kuboresha miundombinu,suala la ajira pamoja na kuboresha sekta ya Maji na elimu .

"Napenda niwaambie wanaarumeru kuwa jembe limekuja nitafanya mabadiliko makubwa ya ajira kwa vijana mimi ndio nimekuja kuleta majibu "

Ends...

Post a Comment

0 Comments