Na Joseph Ngilisho- ARUMERU
MJUMBE wa Kamati ya Afya na Mazingira Ccm Taifa,HILLARY LOISHIYE MOIKAN LESAKWI amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arumeru Magharibi,kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika mchakato unaoendelea nchi nzima.
Wanachama mbalimbali wameendelea kujitokeza kuwasilisha nia yao ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Hillary ni miongoni mwa wanasiasa waliowahi kuwania uteuzi wa nafasi hiyo Jimbo la Arumeru Magharibi,na leo ni mara ya pili kushiriki mchakato huo akiwa na imani kwamba ndoto yake itatimia na hatimaye akapata uteuzi katika jimbo hilo ambalo mpaka sasa lina watia nia zaidi ya 10 waliochukua fomu.
"Nimesukumwa kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Arumeru Magharibi kwa ajili ya kwenda kuwasemea wananchi wa jimbo hilo kuhusu maendeleo ya Afya ,Elimu , Barabara na kazi ya mbunge ni pamoja na kuwa daraja la wananchi ili kusukuma maendeleo".Alisema.
0 Comments