Na Joseph Ngilisho-ARUMERU
DAKTARI Ojung’u Ole Saitabau ni miongoni mwa makada 15 wa CCM waliojitosa Kugombea Uteuzi wa Ubunge jimbo la Arumeru Magharibi Mkoa wa Arusha.
Ojung'u ambaye pia ni mwanasayansi mbobezi wa masuala ya Jografia na maendeleo, ameibuka rasmi leo na kuchukua fomu kama mmoja wa wagombea wa nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Arumeru Magharibi, akiahidi kuleta mageuzi ya kweli ya kiuchumi na maendeleo jumuishi kwa wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Arumeru Magharibi, Dkt Ojung’u amesema uamuzi wake unatokana na mwito wa muda mrefu wakuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi .
Alidai kuwa akiwa mbunge kama atapatiwa ridhaa hiyo kupitia chama cha Mpainduzi atahalikisha jimbo hilo linakuwa na maendelwo ya dhati tofauti na lilivyo kwa sasa.
0 Comments