ESTER MOLLEL MWANAMKE PEKEE AJITOSA KUWANIA UBUNGE ARUMERU MAGHARIBI NI MSOMI WA TAALUMA YA UHASIBU

Na Joseph Ngilisho-ARUMERU

KADA wa Chama Cha Mapinzuzi CCM na mjasiriamali mwenye taaluma ya uhasibu, CPA Ester Mollel, amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa  kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Ester anakuwa mwanamke wa kwanza kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo  katika  Mkoa wa Arusha akiunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu ya kuwataka wanawake wasiogope kugombea majimbo ya uchaguzi, tofauti na wanawake wengi wanaoomba kwenye viti maalumu.


Ends..

Post a Comment

0 Comments