By arushadigtal-DAR ES SALAAM
Mvutano mkali wa kisheria waibuka katika kesi ya tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, baada ya upande wa Jamhuri kuomba ahirisho kwa sababu umewasilisha maombi ya kuficha mashahidi katika kesi hiyo.
Aidha, umeeleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwamba hawawezi kusema wanawaficha mashahidi hao 15 kwa sababu gani kutokana na kwamba maombi yao yamefungiliwa mbele ya hakimu mwingine.
Taarifa hiyo ilitolewa leo june 2,2025 na Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Geofrey Mhini kwa kuomba ahirisha hadi pale maombi yao waliyoyawasilisha mahakamani hapo yasikilizwe na kutolewa uamuzi, hoja zilitolewa kuanzia saa 8:05 mchana hadi saa 11:7 jioni umauzi ulipotolewa.
"Mheshimiwa upande wa Jamhuri tunaomba ahirisho la kesi hii kwa sababu tumewasilisha maombi ya kulindwa kwa mashahidi chini ya Kifungu cha 188 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na Kifungu cha 392 (A) cha CPA katika Mahakama hii,"amedai Wakili Katuga
Amedai kuwa maombi hayo yenye kumbukumbu namba 13298/2025, kwamba uamuzi wa Mahakama kuhusu maombi hayo unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mwenendo wa kesi nzima, hivyo waliomba shauri hilo la jinai liahirishwe ili kutoa nafasi ya kusikilizwa kwa maombi hayo.
Wakijibu ombi hilo, jopo la mawakili 30 wanaomtetea Lissu walipinga maombi hayo wakidai kwamba ni njama ya kuchelewesha haki na kuendesha kesi kwa usiri usio na msingi wa kisheria.
“Hatuwezi kuahirisha kesi kusubiri tukio ambalo halijatokea. Huu si msingi wa sheria. Kama hawapo tayari kuendelea, Mahakama ifute mashtaka na imuachie mshtakiwa,” amedai Wakili Jeremiah Mtobesya.
Wakili Peter Kibatala ameibua hoja kuwa mahakama tayari ilikuwa imetoa amri ya kupewa maelezo ya mlalamikaji kutoka kwa upande wa mashtaka, lakini hadi sasa hawajapokea chochote licha ya kuwasilisha barua mbili zilizosainiwa na kupokelewa katika ya ofisi ya DPP.
“Tunauliza, huu ndiyo msimamo wa DPP? Kama sisi tungedharau amri ya Mahakama, ingekuaje?, lazima amri za Mahakama ziheshimiwe ilisema tupewe maelezo hayo lakini hatujapewa” amehoji Kibatala
Pia, amedai kwamba mawakili wa Serikali walijisahaulisha kabisa kuhusu amri iliyotolewa kwa mara ya mwisho wao kama na mambo mengine ambayo yazuii kesi hii kuendelea kwa mashahidi wa upande wa Jamhuri.
Wakili Dk Rugemeleza Nshalla ameonya kuwa kuzunguka zunguka na kuchelewesha mwenendo wa kesi kunawafanya wananchi kuona kama kuna mambo yanayofichwa na kudai kuwa hawajawasilusha sababu za kutosha za kuomba ahirisho.
Kwa upande wao, Jamhuri wamesisitiza kuwa maombi yao ni ya kisheria, na kwamba yanahitaji kusikilizwa kabla ya mashahidi kuwasilishwa, kwa kuwa uamuzi wa Mahakama kuhusu maombi hayo yanaweza kubadilisha kabisa mwenendo wa shauri.
Wakili Katuga ameendelea kudai kwamba kuna hoja nyingi za kuvunjwa haki za kikatiba, lakini hakusema sehemu Mahakama imetamka hivyo, kama ni hivyo wao wanatakiwa kwenda Mahakama Kuu kufungua kesi ya Kikatiba.
"Sijui wanag'ang'ania taarifa za mashahidi za nini huyu ni mtoa taarifa. Kama DPP ataona shahidi anatakiwa kulindwa analeta maombi ndivyo alivyofanya. Kesi haiwezi kufutwa kwa sababu mlalamikaji yupo na ni Jamhuri,"
Wakili Katuga alidai kuwa wao wanachokiomba ni ahirisho tu hicho ndiyo wanaomba kifanyike na kuhusu kwa nini wanafichq mashahidi watazungumzwa kwenye maombi hayo.
Kuhusiana na wao kupewa maelezo ya mlalamikaji, Wakili Katuga amedai kuwa kama.shshidi huyo.wtamtumia kama shahidi basi watapewa na pia sheria inawataka wafanye hivyo
"Yeye alielezwa na mtu aliyepeleka barua ofisi kwamba hawatapewa maelezo hayo inqoneka kabisa hajasikia mwenyewe na masikio yake kutoka ofisini kwetu, kwa sababu barua ilivyoandikwa haiwezi kujibiwa kwa mdomo, kwa hiyo imebaki kwamba aliambiwa,"amedai
Akimalizia kwa kudai kuwa, hoja zote zilizotolewa hazijazuia Mahakama kutumia busara zake kwa kutoa ahirisho, lakini pia mawakili.wa utetezi wanajua kwenye mioyo yao ni kwanini wanawaficha.
Hakimu Mhini ameanza kuandika uamuzi kuanzia saa 10:28 jiioni hadi saa 11:7 jioni alipotoa uamuzi kwamba kwa busara ya Mahakama anaiona ni bora aahirishe kesi hiyo, kwa hiyo amekubaliana na hoja za upande wa utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Juni 16,2025.
Ilidaiwa kuwa Aprili 3,2025 jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa na lengo la kulagai umma alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube ambapo maneno hayo yalisomeka 'Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana , wagombea wa Chadema walienguliwa kwa melekezo ya Rais'.
Maneno mengine yalisomeka ' Mapolisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi, pia alichapisha maneno yaliyosomeka Majaji ni Ma-CCM hawawezi kutenda haki wanapenda wapate teuzi kuchaguliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa,'
Katika hatua nyingine Tundu Lissu amesababisha malumbano makali ya mawakili wa pande zote mbili katika kesi ya tuhumaza Uhaini, baada ya kutamka kauli ya 'No reforms no Election' ndani ya chumba cha Mahakama bila kujali kwamba hakimu yupo ndani.
Kauli hiyo hiyo ambayo iliambatana na ombi la ahirisho la kesi hiyo kutokana na upelelezi kutokukamilika ilichukua zaidi ya saa mbili kuanzia saa 10:15 asubuhi hadi saa 6:21 mchana na uamuzi kuaomwa hadi 7:12 mchana, na baada ya kusikiliza pande zote mahakama ilimuonya Lissu na wafuasi wake dhidi ya kauli za kisiasa.
Lissu akiwa amezungukwa na askari wa Jeshi la Magereza zaidi ya sita akiingizwa katika kizimba cha Mahakama huku Hakimu Mkazi Mfawidhi Franco Kiswaga akiwa ameketi katika kiti chake, aliinua mkono wake juu na kutamka maneno, 'No Reforms no Election'.
Kauli hiyo iliamsha wafuasi wa chama hicho waliyokuwepo katika chumba jicho kwa kuitikia kauli hiyo kwa kuirudia tena, ambapo Lissu aliinua mkono wake huku akionesha ishara ya vidole viwili ambayo iliungwa mkono na baadhi ya wanachama na wao wakaonesha ishara hiyo.
Hali hiyo ilisababisha, Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga kuwasilisha ombi mbele ya Mahakama, alidai kuwa kauli hiyo ya mshtakiwa mbele ya Hakimu na dharau na pia inavunja heshima ya Mahakama ambayo inategemewa itende haki
Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala, alipinga hoja zote mbili, akisema hakuna kosa lililofanyika kwa maneno ya “No reforms, No election” aliyotamka Lissu kwa sababu si matusi.
Katika kesi hiyo, Lissu aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh milioni tano na Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
0 Comments