MADIWANI WAAGA RASMI JIJI LA ARUSHA BAADHI WAKINUNA,WACHEKELEA KUACHIWA VISHKWAMBI,WAZIRI MCHENGERWA ATOA NENO ,RC MAKONDA ATAKA WALIPWE MAFAO YAO CHAP!

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 


Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amevunja rasmi mabaraza ya Madiwani hapa nchini na kuwashukuru madiwani kwa kufanya kazi iliyotukuka na kusema kuwa kazi yao imeandikwa kwenye kitabu cha dhahabu.

Aidha waziri Mchengerwa ameamuru madiwani kote nchini waliopatiwa vitendea kazi vya serikali ikiwemo vishkwambi kubaki navyo na hawatapaswa kuvikabidhi kwenye halmashauri zao.


"Maelekezo yangu kwa katibu mkuu wa TAMISEMI vifaa hivyo walivyokuwa wakivitumia madiwani kama vitendea kazi wabaki navyo kwa sababu humo ndani wameweka mambo yao na sio sehemu ya mali za halmashauri"


Mchengerwa ametoa kauli hiyonleo juni 20,2025 wakati akiongea kwa njia ya simu na baraza la madiwani la jiji la Arusha kupitia mkuu wa mkoa wa Arusha Paulo Makonda baada ya kumuunganisha na kusema kuwa kauli hiyo ameisema kwa niaba ya mabaraza yote nchini ambayo yanakoma leo juni 20,2025.

"Nakushukuru sana mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kuniunganisha na baraza la madiwani la Arusha na kufanya iwe kituo cha kutoa tamko kwa mabaraza yote nchini"


Waziri Mchengerwa  aliwashukuru Mameya pamoja na wenyeviti wote wa halmashauri nchini na kusema kuwa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita yametekelezwa vyema chini ya mamlaka za tawala za Mikoa na serikali za Mitaa kupitia mabaraza hayo ya madiwani.


"Hii maana yake msingi wa kazi kubwa ya nguvu na jasho ,ufundi na stadi ambao umefanywa na madiwani kote nchi nzima wakizisimamia vema halmashauri zetu nchini"


"Hivyo niwapongeze mameya na manaibu meya ,wenye viti wa halmashauri za miji na wilaya kazi yao imeandikwa kwenye kitabu cha dhahabu kwa sababu wameitumikia nchi hii pamoja na wananchi wanyonge"Alisema waziri.

 Kwa mujibu wa Mchengerwa,  mafanikio yote  yanayoandika sasa na  serikali ya awamu ya sita hasa katika utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na serikali za mitaa, ni mafanikio ya pamoja kati  ya serikali kuu na serikali za mitaa ambayo yamesimamiwa  kikamilifu na na madiwani kote nchini.

Awali Mkuu wa mkoa wa Arusha Paulo Makonda aliwaasa madiwani kwenda kusimamia amani kwenye kata zao na wasikubali kuona vurugu ya aina yoyote inatokea na  wasiwe chanzo cha virugu kwa watakao shindwa kurudi kwenye mafasi zao za udiwani katika uchaguzi ujao.


Pia Makonda alisisitiza kwa Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,John Kayombo pamoja na wakurugenzi wengine katika mkoa wa Arusha  kuhakikisha wanalipa stahiki za Madiwani kwa wakati ili watumie fedha hizo kwa majukumu yao ya kisiasa na mengineyo.


Aliwaomba kwenda kuyatangaza mema yote yaliyofanywa  na serikali chini ya rais Dkt Samia Suluhu hasani ambaye amekuwa mwanamageuzi wa kiuchumi nchini.

 







Makonda pia aliagiza wenyeviti wote wa serikali za mitaa na kitongoji kuhakikisha wanapata malipo yao kwa wakati kupitia akaunti zao na sio kutoa fedha kwa mtendaji wa kata ili awalipe na pia washirikishwe kikamilifu katika miradi ya maendeleo ya halmashauri .


"Hii itaongeza utendaji kazi na sio mpaka ukamchekee chekee mtendaji wa kata ndo upate pesa yao ,hilo jambo halikubaliki"

 

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude  amewataka madiwani hao wanaomaliza muda wao kuendelea kusemea kazi za serikali zilizofanywa na Rais Samia Hassan Suluhu katika kila kata za Jiji hilo. 


Amesisitiza miradi isiyokamilika serikali itasimamia ikiwemo kivuko kiaichojengwa ilhali fedha zipo kwenye akaunti kata ya Ferrari, Osunyai korongo inasemekana mkandarasi kaondoka bila kujenga hivyo yeye  hatakuwa mpole, atahakikisha kazi site zilizopaswa kumalizwa zitasimamiwa


Awali mkurugenziwa Jiji la Arusha, John Kayombo amewataka madiwani wa Jiji la Arusha kutoka kata zote  25 waliomaliza muda wao wa udiwani kutumia baraza hili kuaga na si kuomba miradi 


"Ageni msiombe miradi, tumieni baraza hili kuagana na kushukuru kwa kukaa katika baraza hili kwa miaka mitano tunatamani mrudi kama mlivyo basi tuwatakie kila la heri,"alisema

Mmoja ya madiwani wa viti maalumu ,Veronica Hosea aliishukuru halmashauri pamoja na watendaji wote  kwa ushirikiano walioupata na kufanya wafikie hapo walipo fikia katika kutekeleza majukumu ya maendeleo kwa wananchi katika halmashauri hiyo.










Ends...






Post a Comment

0 Comments