Breaking News: Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima limefungiwa kwa kosa la kutumika Kisiasa.
By arushadigtal
Barua kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Ofisi ya Msajili wa Jumuiya inasomeka kama ifuatavyo:-
KUFUNGWA KWA SHUGHULI ZA KANISA LA GLORY OF CHRIST CHURCH - KANISA LA UFUFUO NA UZIMA
Chini ya Kifungu cha 17(b) na kifungu cha 2 cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337 kama kilivyorekebishwa na kifungu cha 39(b) cha Sheria ya Marekebisho Mbalimbali ya Sheria Namba. 3 ya Mwaka 2019
Tafadhali, rejea somo tajwa hapo juu.
2. Katika siku za hivi karibuni, kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, umeonekana ukiwa katika mimbari ya Kanisa la Glory of Christ Church @ Kanisa la Ufufuo na Uzima, ukitoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi. Vitendo hivi ni kinyume cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337na vinaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.
3. Kwa Mamlaka niliyopewa, Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia inafuta usajili wa Glory of Christ Church @ Kanisa la Ufufuo na Uzima, kuanzia leo tarehe 02 Juni 2025. Hivyo, unatakiwa kusitisha shughuli za Kanisa lako mara moja.
4. Chini ya kifungu cha 19(1) cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, Kanisa lina haki ya kukata rufaa juu ya uamuzi huu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia kwa Katibu Mkuu, ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya barua hii.
5. Kwa Amri ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia.
Ends....
0 Comments