Watu 37 wafariki kwenye ajali ya basi mkoani Kilimanjaro
By arushadigtal-SAME
Watu 37 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea leo, Juni 28, 2025, katika eneo la Sabasaba, Kata ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi la kampuni ya Channel One lililokuwa likitoka Moshi kuelekea Tanga kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likisafiri kutoka wilayani Same.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, magari yote mawili yalishika moto mara baada ya kugongana, na juhudi za uokoaji zinaendelea katika eneo la tukio.
“Mpaka sasa, tumethibitisha vifo vya watu 37, huku wengine 30 wakiwa wamejeruhiwa. Vikosi vya uokoaji bado vinaendelea na kazi ya kuwaokoa manusura na kuondoa miili ya waliopoteza maisha,” amesema Babu.
0 Comments