RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU,AMTUPA NJE DORIYE WA NGORONGORO

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Abdul-Razak Badru, kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA). 

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Badru alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), anachukua nafasi ya Dkt. Elirehema Joshua Doriye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia Rais Samia amemteua Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kabla ya uteuzi huu, Dkt.
Nyansaho alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania.


Post a Comment

0 Comments