Na Joseph Ngilisho MERERANI
WACHIMBAJI watatu wadogo wa madini ya Tanzanite (Wanaapolo) Mererani ,wanahofiwa kufa kwa kufukiwa ndani ya migodi ya madini katika mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Hii imefahamika mara baada ya famili zao kutowaona jamaa zao kwa muda wa takribani wiki mbili na kuanza kuwatafuta na kuamua kuandamana katika lango kuu la Mererani wakitaka kupata taarifa zaidi juu ya ndugu zao.
Taarifa za kutoonekana kwa wanaapolo hao zilianza kuzagaa katika viunga vya migodi hiyo ya Mererani kuanza aprili 12 wiki iliyopita huku ndugu wa jamaa hao wakionekana kulizonga lango kuu la Mererani wakitaka kujua ndugu zao wako wapi.
Hawa Mbega ni mmoja ya familia anayemtafuta mume wake aitwaye,Frank Mekoki ambaye alidai hajamwona kwa muda wa siku 17 tangu siku ya idd alipomuaga anaenda mgodini.
"Ninachoomba serikali isaidie kupatikana kwa mume wangu awe hai ama amekufa kwa nini wanafichaficha ,maana tunawasiwasi kama mwenye mgodi amewatoa kafara,kwanini mwenye mgodi hataki watu waingie kwenda kuwatafuta"
Alisema hadi sasa serikali haijatoa taarifa kamili inafichaficha tunamwomba Rais Samia Suluhu Hasan aingilie kati
"Tunaomba mwenye mgodi afunguke atuoneshe ndugu zetu wapo wapi ,wamewazuia vijana wasiende kuwatafuta ,tunaomba waruhusiwe wakawatafute tena kwanini anafichaficha"Alisema Veronica Joseph ndugu wa watu hao.
Taarifa zaidi zinadai kwamba wanaapolo hao walizama shimoni(mgodini)wakiwa tisa kwa njia ya panya katika mgodi mmoja wapo Mkubwa kwa lengo la kuchukua madini ila walikosa hewa na kutoonekana hadi sasa.
Katika kikao kilichoketi jumamosi na jumatatu katika ofisi ya Afisa mfawidhi wa Madini Mererani RMO,hoja kubwa ni namna ya kupata taarifa za wachimbaji hao ambao hawakuwa sehemu ya wameajiriwa katika migodi inayohofiwa kufia watu hao.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Fakii Raphael Lulandala amethibitisha kuwepo kwa taarifa za kupotea kwa wachimbaji hao na kudai kwamba jitihada za kuwasaka katika migodi kadhaa inayohofiwa kufanya kazi kwa watu hao zimefanyika ila hadi sasa bado hawajaonekana tangu taarifa hizo ziwafikie aprili 12,Mwaka huu .
"Tupo katika zoezi la kuwasaka watu hao ,ambao zipo hisia kwamba wamefia migodini ,hadi sasa hatujapata ukweli hadi wapatikane ,ipo migodi mikubwa wanayohofiwa kuwa waliingia ndanii na upekuzi umefanyika na unaendelea"
Mkuu huyu wa wilaya ambaye hakuwa tayari kuweka wazi migodi hiyo ,alisema kuwa bado vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa jambo hilo na taarifa zaidi zitatolewa baada ya kukamilisha uchunguzi.
Kutokana na taarifa hizo kuzagaa katika mgodi huo wa Mererani,hofu imetanda katika machimbo hayo huku baadhi ya migodi inayohofiwa watu hao kuinga kinyemela ikitajwa na kuitaka serikali kuongeza uchunguzi ili kuwapata watu hao.
Vyanzo mbalimbali vya habari kutoka Mererani vimeeleza kuwa Hali ya hewa ilichafuka baada ya baadhi ya wachimbaji kuokota nguo za baadhi ya viatu vya wachimbaji hao ambapo walianzisha tafrani Kwa kuitaka serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini miili ya wachinbaji hao wanaohofiwa kufariki.
Taarifa hizo zimeenda mbali zaidi na kudai kwamba mara baada ya tafrani hiyo serikali iliamua kutoa kibali Kwa wachimbaji hao kuzama katika moja ya migodi mikubwa inayotajwa, kwa lengo la kuwasaka wachimbaji hao, lakini jitihada hizo hazikuzaa matumda.
"Unajua baada ya kuona siku zinaenda na hawajawaona wenzao wachimbaji wakaanza kuleta fujo pale ofisi za wi,ara ya madini na ndipo walipopewa kibali Cha kuzama kwenda kuwasaka wenzao kwenye migodi hiyo"kilieleza chanzo muhimu cha habari
End....
0 Comments