Na Joseph Ngilisho Arusha
WAKUU wa Idara za Utawala na Rasilimali watu Katika Utumishi wa Umma, wameambiwa kwamba Moja wapo ya sifa ya Utumishi uliotukuka ni kujifunza na kusikiliza changamoto za watumishi waliopo chini yao na kuzitatua badala ya kukumbilia kufanya mabadiliko ya haraka haraka kwenye taasisi walizopangiwa au kuhamishwa.Hayo yameelezwa Oktoba 13 na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Katiba na Sheria Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Haroun Ali Suleimani,alipokuwa akifunga kikao kazi kilichodumu kwa siku tati kwenye Ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC Jijini Arusha.
Watumishi wanapopewa vyeo watambue kuwa wameongezewa majukumu na sio upendeleo.
Alisema kwanza Maafisa hao wanatakiwa kujitambua wao ni nani Katika dhamana yao waliyonayo Katika kutoa huduma kwa umma.
Alisema moja wapo ya sifa iliyotukuka ya Utumishi ni pamoja na kutokufanya mabadiliko ya haraka wanapopewa majukumu kwanza wajifunze ,wasikilize watumishi waliopo na waache tabia ya kukaripia karipia haifai badala yake wazingatie maadili.
Alisema Utumishi wa umma una mambo manne ambayo ni Uzalendo,ambapo lazima wawe watiifu Kwa nchi ,wenzao Kwa kuwa cheo sio zawadi bali ni majukumu wawe na lugha ya upole.
Jambo lingine ,amewataka wasiamini waliopo chini yao Kwa asilimia 100 ,akawasisitiza wazungumze na watumishi wawasikilize matatizo yao na kero zilizopo wazipatie ufumbuzi.
Kauli mbiu ya kikao hicho inasema Usimamizi wa raslimali watu unaozingatia maadili ,Sheria,uwajibikaji na matumizi ya Tehama, ni msingi wa utoaji huduma bora Katika Utumishi wa umma.
0 Comments