Na Joseph Ngilisho Arusha
SHULE yenye mchepuo wa kiingereza ya St MARGARET'S ACADEMY ipo mbioni kuanzisha shule ya sekondari na chuo cha ufundi katika eneo la Nduruma wilayani Arumeru Mkoani Arusha ikiwa ni mpango wake wa kuwasogezea karibu huduma ya elimu watoto wenye uhitaji waliopo eneo hilo.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa shule hiyo Honest Tesha katika mahafali ya 21 ya darasa la saba na kueleza kuwa ujenzi wake umeanza baada ya kupata eneo lenye ukubwa wa ekari 70 na wanatarajia ifikapo 2025 waanze kuchukua wanafunzi.
Tesha aliwashukuru wazazi kwa ushirikiano wao uliowezesha watoto kuhitimu wakiwa na afya njema ,aliwasihi kuendelea na moyo huo ili kumwezesha mtoto kupata elimu bora.
Alisema shule ya St MARGARET'S imeamua kupanua wigo wa elimu kwa kujenga matawi ya shule ikiwemo kuanzisha tawi la shule hiyo wilayani Monduli litakalowasidia wanafunzi wengi wanaotoka wilayani humo kufuata shule hiyo wilayani Arumeru.
Kwa upande wake Meneja wa benki ya CRDB tawi la Clock Tower jiji Arusha Aika Mawala ambaye alikuwa mgeni rasimi wa mahafali hayo aliwataka Wazazi na walezi kurudi kwenye misingi ya malezi ili kuwaepusha watoto dhidi ya mmomonyoko wa maadili unachagiwa na athari ya kukua kwa utandawazi .
Meneja huyo ambaye aliwatunuku vyeti wahitimu 83, aliwataka kuzingatia waliyojifunza ikiwemo maadili ili yawasaidie atika masomo yao ya mbeleni na kuachana na mambo ya kidunia ikiwemo kuiga tamaduni za kigeni
.
Aliwashauri wazazi kuwajengea watoto tabia ya kuwafungulia akaundi kwenye benki ili kuwapa nidhamu ya matumizi ya fedha hali itakayosaidia mtoto kujiepusha na maumizi yasiofaa.
Naye makamu Mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo na makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha DC wilayani Arumeru,Fred Lukumay alisema halmashauri ya Arusha Dc inajivuniwa uwepo wa shule hiyo ambayo imekuwa ikifanya vizuri kiwilaya na Kimkoa.
Aidha alitoa rai kwa wazazi wa jamii ya kifugaji kuacha tabia ya kuwabagua watoto wa kike katika kuwapatia elimu bora na kuwataka wahakikisheb wanawapa elimu iliyo sawa ili kutimiza ndoto zao.
"Niwaombe wazazi katika kipindi hiki watoto wao wamehitimu masomo wapo wajumbani, waongeze ulinzi kutokana na vitendo vya ubakaji ,ulawiti na ukatili kushamiri"
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Michael Magaya alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2003 ikiwa na wahitimu watatu na wanajivunia kuona shule ikiendelea kuaminiwa na kupiga hatua na leo mwaka 2023 wanafunzi wapatao 83
Wamehitimu masomo yao.
Alisema St MARGARET'S ACADEMY imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya ngazi ya wilaya na Mkoa na wanampango wa kuanzisha tawi lingine wilayani Monduli ili kuwarahisishia watoto wanaotoka wilaya humo .
Ends...
0 Comments