DED HAMSIN ATOA ONYO KALI KWA WATUMISHI WENYE MIDOMO KAMA KASUKU 'MSEMAJI WA HALMASHAURI NI MKURUGENZI NA MEYA' AKERWA NA TAARIFA POTOFU ZA MIRADI YA MAENDELEO MKUU WA KITUO CHA AFYA AKALIA KUTI KAVU

Na Joseph Ngilisho ,Arusha 

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuacha kushiriki majungu yanayogombanisha chama na Serikali.


Mhandisi Hamsini ameyasema hayo mwishoni mwa wiki katika ziara ya kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Arusha Jiji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Wilfred Soilel iliyokuwa ikitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Jiji la Arusha.


Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja naKituo cha Afya cha Levolosi,Shule ya Wasichana ya Arusha Girls,Barabara ya Engosheraton sambamba na eneo Bondeni City inapojengwa stendi ya mabasi ya Mikoani.


"Yamesemwa maneno mengi sana kuhusu miradi hii mimi kama Mkurugenzi Natoa onyo kali kwa watumishi wangu msemaji wa Halmashauri ya jiji la Arusha ni meya na Mkurugenzi wake pekee."Alisema.


Hata hivyo Mkurugenzi aliendelea kuongezea kuwa mradi huo fedha zake zilikuja tangu mwaka 2022 fedha na hazikuwa kwaajili ya kituo cha  Afya Levolosi bali ni kwaajili ya kituo cha Afya kaloleni ila kwa busara na hekima za  Baraza la madiwani waliomba baadhi ya fedha zipelekwe levolosi kwaajili ya ujenzi na maelekezo ya Tamisemi kupitia kwa Katibu Mkuu yakiwa yanaelekeza miradi yote ngazi ya chini kutakiwa kufanywa kwa FORCE ACCOUNT.


"Sisi hapa Arusha tunaufinyu wa ardhi ilituweze kutoa huduma bora na majengo mazuri tumekubaliana Halmashauri kwenye vikao vyake halali vya kisheria imekubali kujenga magorofa ya shule pamoja na vituo vya afya na zahanati kwasababu kwa jiji letu hekari moja ni zaidi ya milioni mia moja kupata fidia." Alisema


"Tumeomba kibali Tamisemi tutumie mkandarasi kwasababu gorofa lolote lile lina msingi ya kihandisi ambayo inasimamiwa na CRB na IRB na Institute of Engineering IET,kwahiyo ukienda kinyume huwezi kufika na kama gorofa likiua watu lazima utawajibika"


" Halmashauri tumewaajiri mafundi wetu tunataka watu waliokizi vigezo na kusajiliwa na IRB na CRB kwaajili ya Labour Force ndiyo wanaweza kufanya ujenzi wa magorofa" Alisema Hamsini



Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amesema kuwa Fedha za kujenga kituo cha afya kaloleni zililetwa ila hakukuwa na eneo la kujenga gorofa na kuamua kupeleka fedha hizo katika Kituo cha Afya levolosi .


"Kama kiongozi mwenye dhamana ya wilaya yakusimamia miradi na mambo yote ndani ya Wilaya sikuona sawa kuajiri mkandarasi mwenye bajeti kubwa kuliko kile tulichokuwa nacho na kutafuta mkandarasi mwingine mwenye sifa nakupata majengo yenye ubora na kupata mkandarasi na sasa yuko kazini" Alisema


"Tulisamimisha ujenzi kwa awamu ya kwanza kutokana na ubadhirifu mkubwa wa pesa uliofanyika ambao ulitakiwa kufanyika na ukatufanya kusimamisha ujenzi ilikupata mkandarasi aliyesahihi na tumepata na mpaka sasa tunaendelea na ujenzi." Ameongeza 


Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Timoth Sanga ameipongeza Halmashauri ya jiji la Arusha kwa miradi mizuri na kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama na kuupongeza uongozi wote wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya kwakutekeleza vyema yale yote waliyoyanadi katika uchaguzi mkuu kutokana na maendeleo yanayoonekana ni makubwa na kuwahasa viongozi wa mitaa na madiwani kuendelea kutoa elimu kwa wakazi wa jiji la Arusha. 


Ends....


Post a Comment

0 Comments