NA Joseph Ngilisho ARUSHA
Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo ameapa kuendelea kupambana na mafisadi katika halmashauri ya jiji la Arusha na ameipongeza mahakama kwa kumhukumu kifungo cha miaka 20 aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima ambaye anatumikia kifungo chake katika gereza kuu la Kisongo Arusha.
Gambo ameyasema hayo wakati alipokuwa akizindua kikundi cha maendeleo cha SIMANJIRO FAMILY kilichopo kata ya Sombetini jijini Arusha,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kazi aliyo nayo nikupambana na mafisadi ,kutetea na kulinda maslahi ya wananchi ambao anaamini walimchagua.
"Baadhi ya watu waliniona ni mtu mbaya lakini ukweli unadhihilika mahakama imeamua tumeona haki imetendeka na mtu amefungwa miaka 20 sasa mimi na wao nani mwongo"
Dkt Pima na wenzake wawili aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu walikutwa na hatia kwenye makosa ya uhujumu uchumi na kufungwa miaka 20 kila mmoja.
Hukumu hiyo imetolewa Agosti 31, 2023 Hakimu Seraphin Nsana wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha baada ya kujiridhisha pasina Shaka juu ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kwa pande zote mbili.
Wakati huo huo Gambo alikipongeza kikundi hicho cha Simanjiro family kwa kubuni na kuanzisha kikundi hicho na kuwataka wananchi wengine kuiga mfano huo ili aweze kuwaunganisha na makampuni
Makubwa ya kibiashara
Alisisitiza kuwa ubunifu wa kuanzisha kikundi hicho cha Maendeleo ulenge kuwanufaisha wahusika wote kwa shida na raha ili kujiletea maendeleo na kisitumike kinyume na malengo .
Katika uzinduzi huo Gambo alichangia viti 50 vya biashara na aliwaahidi wanakikundi hao kuwaunganisha na kampuni za kibiashara wawe wakala wa kusambaza bidhaa na faida watakayopata iwasaidie kujiongezea kipato na kuachana na tabia ya kukopeshana fedha inayosababisha mfarakano.
"Mmeonesha nia yenu njema ya kuanzisha kikundi cha maendeleo kama mtanikubalia naomba niwaunganishe na kampuni ya uzalishaji wa gesi za majumbani ili mfanye biashara kama wakala wa kusambaza mitungi hiyo ya gesi na hivyo kunufaika na faida itakayokuwa mkipata".
Awali wanakikundi hao kupitia risala yao iliyosomwa na mwenyekiti wa miradi Bernadeta Changuru walimwelez mbunge huyo kwamba kikundi chao kimeanzishwa mwaka 2020 na kusajiriwa na kimelenga kujikwamua kimaisha kwa kuendesha biashara ya kukodisha viti na mapishi kwenye sherehe.
Alisema hadi sasa Simanjiro Family inajumla ya wanachama zaidi ya 100 na wamefanikiwa kuwa na mtaji wa viti 150 na wamelenga kupata viti 500 kama hatua ya kuanzia mtaji wao na walimwaomba mbunge huyo kuwa mlezi na mwanachama wa kikundi hicho na asaidie kuboresha mtaji wao.
Naye Mwenyekiti wa Simanjiro Family group Bahati Mushi alisema kuwa kikundi chao kimetokana na mtaa wa Simanjiro na kimelenga kusaidiana katika shida na raha na tangu wamekianzishwa kina umri wa zaidi ya miaka mitatu.
Alisema tofauti iliyopo kati yao na vikundi vingine ni kwamba kikundi chao sio cha kukopeshana ila kimejikita zaidi kusaidiana ili1 kukwamuanankiuchuni kutokana na faida watakayoipata kwenye biashara wanayofanya ya kukodisha vitu na kupika vyakula kwenye shereha na msiba.
Ends...
0 Comments