AMATA YAWANOA WASICHANA WA KAZI MAJUMBANI,WAFUNGUKA MAKUBWA ••KUMBE WANATUMWA KUTEKA PENZI LA BABA MWENYE NYUMBA 'UTAJUA HUJUI'

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA

Taasisi ya Ajira na maendeleo Tanzania (AMATA)ya jijini Arusha imewapatia mafunzo wafanyakazi wa majumbani waweze kujitambua na kuthamini kazi yao na kuiona ni ajira kama ajira nyingine inayowaingizia kipato katika dira ya maisha.




Akitoa mafunzo hayo ya siku moja kwa wafanyakazi zaidi ya 30 wa majumbani,mkurugenzi wa shirika hilo,Bernadette Clementi akishirikiana na mume wake Silvester Temba alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wafanyakazi hao waweze kujitambua na kuyafikia malengo yao .

Alisema baadhi ya wafanyakazi wa majumbani wameshindwa kuithamini kazi hiyo kwa sababu za kimtazamo wakiamini kazi za ndani wanafanyia shida nani utumwa .

Mkurugenzi  huyo alisema lengo  lingine ni kujenga mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi hao na waajiri wao ili kuondoa sintofahamu ambayo imekuwa ikijitokeza huku baadhi ya wazazi wakiona wasichana wa kazi ni mzigo.

Akizungumza changamoto zinazowakumba  wafanyakazi wa ndani alisema ni pamoja na waajiri kutowalipa ujira wao kwa wakati ,kubaguliwa wakati wa chakula na kutothaminiwa kwenye familia huku wasichana wa ndani nao walidaiwa ni wajeuri na kiburi kutesa watoto  na kugawa vyakula vya ndani.

Baadhi ya wafanyakazi wa majumbani waliopatiwa nafunzo hayo Blandina Anthony na Naomi Shedrack walieleza namna walivyonufaika na elimu walioipata wakidai kuwa imewasaidia kujitambua na kujua haki zao.

Hata hivyo Naomi Shedrack kutoka Ngaramtoni ameeleza changamoto wanazokumbana nazo akidai baadhi ya wazazi wao huwatuma kuja kushawishi kujenga mahusiano ya kimapenzi na baba mwenye nyumba  ili kuwa mama mwenye nyumba, jambo linalowasababisha mfarakano mkubwa wa kifamilia.

"Wapo wasichana wanaotumwa na mabibi zao au mama zao kwa kupewa hata dawa ili kumshawishi baba mwenye  nyumba wawe na mahusiano ya kimapenzi aweze kumpindua mama mwenye nyumba,hata mimi imenitokea"alisema na kuongeza kuwa

"Kuna baadhi ya wasichana wenzetu wa kazi wanajihusisha na ushirikina na mimi nimeshuhudia mwenzangu tulikuwa tunafanya naye kazi kwa boss mmoja huko Njiro alikuwa akijihusisha na ushirikina sana"

Naye  Silvester John mkazi wa Kisongo alisema kuwa wasichana wengi wanaofanyakazi majumbani baadhi yao hawajitambui ndio maana wengi wao wamekuwa wakifanyakazi bila malengo na kutojua wajibu na haki yao.

Alisema semina hiyo itasaidia kuwafumbua macho ili watambue wajibu wao na kuthamini kazi wanayofanya na kujiepusha na matukio yasiyofaa ili kuisaidia jamii yao na wao kukiendeleza kimaisha 





Ends...

















 

Post a Comment

0 Comments