LUKUMAY ATOA WITO WA AMANI NA UMOJA OLJORO
Na Joseph Ngilisho | ARUMERU
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Dkt Johannes Lukumay, amewapongeza waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mirongoine, Kata ya Oljoro, kwa kudumisha amani na umoja, akiwataka kuendelea kushirikiana katika kuimarisha mshikamano wa jamii.Lukumay alitoa pongezi hizo Novemba 8, 2026, aliposhiriki Ibada ya Jumapili pamoja na waumini wa kanisa hilo, iliyokwenda sambamba na hafla ya uzinduzi wa albamu ya Kwaya ya Einoti.
Katika hafla hiyo, mbunge huyo aliwashukuru waumini na wananchi wa Kata ya Oljoro kwa kuendelea kulinda amani na umoja, akisisitiza umuhimu wa kudumisha mshikamano huo kwa maendeleo ya jamii.
Alisema amani na umoja ni msingi muhimu wa ustawi wa wananchi na maendeleo ya eneo lao.
Ends

Post a Comment