Ad
Breaking🔥

LUKUMAY ASHIRIKI MAFUNZO YA VIONGOZI WA BUNGE DAR WA SALAAM

 LUKUMAY ASHIRIKI MAFUNZO YA VIONGOZI WA BUNGE

Na Mwandishi Wetu | Dar es Salaam

Mbunge wa Arumeru Magharibi, Dkt Johannes Lukumay, anashiriki Kozi Fupi ya Viongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CAPSTONE COURSE), Kundi la 18, inayofanyika katika Chuo cha Ulinzi Tanzania jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yanayofanyika kuanzia Novemba 9 hadi 13, 2026, yanalenga kuwawezesha viongozi wa Bunge kuongeza maarifa na uelewa katika masuala mbalimbali yanayohusu uongozi na majukumu yao ya kibunge.

Ushiriki wa Dkt Lukumay katika mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uwezo wa viongozi katika kutekeleza majukumu yao ya uwakilishi, kutunga sheria na kuisimamia Serikali kwa ufanisi.


Post a Comment

Previous Post Next Post