KIMATI AIPA TUMAINI SENIOR DHAMANA YA KUKUZA ELIMU, MICHEZO, UONGOZI
Avutiwa na bunifu za wanafunzi, aahidi kushirikiana na shule hiyo kusambaza maarifa na uzoefu wake katika shule za umma
Na Joseph Ngilisho | MONDULI
Kimati alisema hayo Novemba 07,2026 wakati wa mahafali ya nane ya Kidato cha Nne na maadhimisho ya miaka 10 ya shule hiyo iliyopo Makuyuni, wilayani Monduli, mkoani Arusha, ambapo alieleza kuvutiwa na bunifu zilizobuniwa na wanafunzi pamoja na programu za kuwaandaa vijana kujitegemea.Alisema maonesho ya bunifu hizo yamethibitisha kuwa elimu inayotolewa shuleni inaweza kuwa nyenzo ya kutatua changamoto za jamii badala ya kubaki katika nadharia za darasani.
Alitaja baadhi ya bunifu alizoziona kuwa ni zile zinazohusu utatuzi wa changamoto za mazingira, matumizi bora ya rasilimali na mifumo ya kiteknolojia inayoweza kuongeza ufanisi katika taasisi, ikiwemo mfumo wa kubaini watumishi wanaokiuka muda wa kuripoti kazini.
"Nilichokiona hapa kimenivutia sana. Hawa ni vijana ambao wameonesha uwezo wa kutumia maarifa na teknolojia kutatua changamoto zinazotuzunguka. Hii inaonesha tunahitaji kuwekeza zaidi katika ubunifu wa wanafunzi," alisema Kimati.
Alisema kutokana na uwezo huo, atashirikiana na uongozi wa shule kuhakikisha uzoefu na maarifa yaliyopatikana katika taasisi hiyo yanawafikia wanafunzi wa shule nyingine, hususan za Serikali, ili kuongeza wigo wa fursa za kujifunza na kukuza vipaji.
Alisema michezo si burudani pekee, bali ni nyenzo ya kujenga afya, kukuza uwezo wa kiakili, kuimarisha umoja na mshikamano, pamoja na kufungua fursa za ajira na kujipatia kipato kwa vijana.
Alisisitiza kuwa shule hiyo inapaswa kutumia mafanikio yake katika michezo kuwasaidia wengine, ili vipaji vya vijana viweze kutambuliwa na kuendelezwa tangu wakiwa shuleni.
Pia alivutiwa na programu ya Beyond Success inayolenga kuwajengea wanafunzi na walimu uwezo wa uongozi, akisema mafunzo hayo yana umuhimu katika kuandaa kizazi chenye kujiamini, nidhamu na uwezo wa kukabiliana na changamoto.
Alisema uongozi bora hauanzi mtu anapopewa nafasi ya madaraka, bali hujengwa tangu akiwa mdogo kupitia mafunzo ya uwajibikaji, usimamizi wa muda, mawasiliano na kufanya maamuzi.
Kutokana na umuhimu huo, aliitaka shule hiyo kuendeleza programu hiyo na kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi kuisambaza katika shule nyingine za Wilaya ya Monduli.
Aidha, aliwataka wazazi kuimarisha ushirikiano na walimu katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao, akisema malezi na mafanikio ya kielimu yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya familia na taasisi za elimu.
Alisema uongozi bora hauanzi mtu anapopewa nafasi ya madaraka, bali hujengwa tangu akiwa mdogo kupitia mafunzo ya uwajibikaji, usimamizi wa muda, mawasiliano na kufanya maamuzi.
Kutokana na umuhimu huo, aliitaka shule hiyo kuendeleza programu hiyo na kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi kuisambaza katika shule nyingine za Wilaya ya Monduli.
Aidha, aliwataka wazazi kuimarisha ushirikiano na walimu katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao, akisema malezi na mafanikio ya kielimu yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya familia na taasisi za elimu.
Aliwahimiza wahitimu kutumia elimu waliyoipata kuwa watu wenye maadili, nidhamu na uwajibikaji, akionya dhidi ya kujiona bora kuliko wengine kwa sababu ya kiwango cha elimu walichofikia.
Miaka 10 ya Tumaini
Alisema shule hiyo ilianzishwa ikiwa na malengo makuu matatu ambayo ni kutoa elimu bora, kuwaandaa vijana katika taaluma mbalimbali na kuwajengea uwezo wa kujiajiri.
Bayo alisema mafanikio hayo yanaonekana kupitia maendeleo ya kitaaluma, ushiriki wa wanafunzi katika mashindano ya michezo kuanzia ngazi ya wilaya hadi Afrika Mashariki na uwezo wa wanafunzi kubuni mifumo inayoweza kutatua changamoto za kijamii.
Alisema maonesho yaliyofanyika katika maadhimisho hayo yalionesha ujuzi wa wanafunzi katika matumizi ya kompyuta, mifumo ya taarifa za kijiografia (GIS), ujasiriamali, ufugaji na teknolojia mbalimbali.
"Hatupendi mwanafunzi anapohitimu awe amebeba cheti pekee. Tunataka awe na maarifa na ujuzi ambao utamwezesha kujiajiri, kutatua changamoto zinazomzunguka na kusaidia jamii yake," alisema Bayo.
Alisema shule hiyo pia inajivunia wahitimu walioendelea na masomo ya juu na wengine kuhitimu na kuajiriwa katika taasisi mbalimbali, akitolea mfano mhitimu ambaye sasa ni Meneja wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema mafanikio hayo yanaipa shule motisha ya kuendelea kuwekeza katika elimu inayounganisha maarifa ya darasani na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na maendeleo ya taifa.
Maadhimisho hayo yaliambatana na mahafali ya nane ya Kidato cha Nne, ambapo wahitimu walitunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kwa kutambua juhudi zao, huku shule hiyo ikiadhimisha muongo mmoja wa utoaji wa elimu na malezi kwa vijana.
Ends




















Post a Comment