Ad
Breaking🔥

NJOMBE: MWANAUME AJINYONGA HADI KUFA BAADA YA KUNYIMWA UNYUMBA ,SHARTI MPAKA AOKOKE

NJOMBE: MWANAUME AJINYONGA HADI KUFA BAADA YA KUNYIMWA UNYUMBA ,SHARTI MPAKA.AOKOKE

Na Joseph Ngilisho | NJOMBE

NJOMBE. Mkazi wa Mtaa wa Kambarage, katika Halmashauri ya Mji wa Njombe, Damas Mgaya (38), amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chake, huku uchunguzi wa awali wa polisi ukihusisha tukio hilo na madai ya mgogoro wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi.

Kwa mujibu wa Kamanda Banga, marehemu alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya kiatu iliyokuwa imefungwa kwenye nondo ya dirisha la chumba chake.

Amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo linadaiwa kufuatia kutokuelewana kati ya marehemu na mkewe kuhusu masuala ya ndoa na tendo la ndoa.

Inadaiwa kuwa mke wa marehemu alikataa kushiriki tendo la ndoa, akieleza kuwa mumewe hajaokoka, jambo linalodaiwa kuchangia mgogoro huo wa kifamilia.

Hata hivyo, mazingira hayo ni madai ya awali yanayohitaji kuthibitishwa kupitia uchunguzi wa mamlaka husika.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Banga amewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa mafundisho yanayojenga amani, maelewano na mshikamano ndani ya familia na jamii kwa ujumla.



Amesisitiza umuhimu wa kutafuta suluhisho la migogoro ya kifamilia kwa njia ya mazungumzo na ushauri kutoka kwa watu wanaoaminika, badala ya kuruhusu kutokuelewana kuendelea bila kutafutiwa ufumbuzi.

Aidha, amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kwa vitendo vinavyokiuka sheria.

ARUSHA DIGITAL UPDATE

Post a Comment

Previous Post Next Post