Ad
Breaking🔥

MBUNGE LUKUMAY AWATEMBELEA WATOTO YATIMA ARUMERU ,AWAFARIJI KWA KUWAPATIA ZAWADI MBALIMBALI

LUKUMAY AWAFARIJI WATOTO YATIMA ARUMERU

Na Joseph Ngilisho | ARUMERU

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lembulung Lukumay, amewatembelea na kuwafariji watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Jane Olevolos Orphanage Centre, kilichopo Kijiji cha Olevolos, Kata ya Kimunyak, mkoani Arusha.

Katika ziara hiyo iliyofanyika leo, Oktoba 17, 2026, Dkt. Lukumay aliwapatia watoto hao mahitaji mbalimbali, yakiwemo nguo zilizotolewa na wasamaria wema kutoka Berlin, nchini Ujerumani, akiwemo Dkt. Ursula.

Ziara hiyo inalenga kuwafariji watoto hao, kuwapa faraja na kuonesha mshikamano wa kijamii kwa watoto wanaoishi katika mazingira yenye uhitaji wa upendo, malezi na msaada kutoka kwa jamii.

Ushirikiano kati ya viongozi, wadau na wasamaria wema ni muhimu katika kusaidia kuboresha ustawi wa watoto yatima na kuhakikisha wanapata mahitaji yanayochangia makuzi na maendeleo yao.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم