Ad
Breaking🔥

DC TAMBO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MRADI MZITO WA BARABARA YA KWA GIRIKI SAKINA..WAZEE WA KIMASAI WAMBATIZA JINA JIPYA

DC TAMBO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MRADI MZITO WA BARABARA YA KWA GIRIKI SAKINA..WAZEE WA KIMASAI WAMBATIZA JINA JIPYA 

…Aanza msako wa miradi iliyokwama, atangaza ukaguzi Oktoba 18 na 19

Na Joseph Ngilisho | ARUSHA


MKUU wa Wilaya ya Arusha, Nicodemas Tambo, amewaonya wakandarasi wanaochelewesha miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali, akitangaza kuanza ukaguzi wa miradi hiyo Oktoba 18 na 19, mwaka huu, ili kubaini sababu za ucheleweshaji na kuwawajibisha watakaokiuka mikataba.

Tambo alitoa kauli hiyo Oktoba 12, 2026, wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Giriki hadi Mathias Manga, Kata ya Sakina jijini Arusha, yenye urefu wa kilomita 1.5 na thamani ya Sh milioni 950.

Alisema amepokea maelekezo ya kuhakikisha miradi yote ya Serikali inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi, akieleza kuwa baadhi ya wakandarasi wamelipwa fedha lakini hawajakamilisha kazi walizopewa.





“Nimepata taarifa kuwa kuna wakandarasi ambao wamelipwa fedha za Serikali lakini hawajamaliza miradi yao. Nitaenda kukagua miradi hiyo ili kujua sababu za kutokamilika kwake,” alisema Tambo.

Meya aonya kuhusu kasi ya ujenzi

Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe, amewataka wakandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya barabara ili ikamilike kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.

Iranghe pia aliwataka wananchi kutotupa taka kwenye mifereji ya maji ya mvua itakayojengwa kando ya barabara hiyo, akisisitiza umuhimu wa kulinda miundombinu hiyo ili iweze kufanya kazi iliyokusudiwa.

Mkandarasi wa mradi huo, Jiangxi-Ge Engineering Group Corporation Ltd, ameahidi kukamilisha kipande kilichosalia cha mita 400 kwa kuzingatia muda na ubora unaotakiwa.

Ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, pamoja na kuchochea biashara katika eneo la Sakina na maeneo jirani.

Wakati huohuo, Tambo amewataka wakazi na wafanyabiashara wa Arusha kujiandaa kutumia fursa za kiuchumi zinazotokana na maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, akitaja sekta za malazi, chakula, usafiri na utalii kuwa miongoni mwa zitakazonufaika.






Ends

Post a Comment

أحدث أقدم