CHIVAYO NA MKEWE KUZIKWA PAMOJA ALHAMISI
Na Joseph Ngilisho | HARARE, ZIMBABWE
MFANYABIASHARA maarufu nchini Zimbabwe, Wicknell Chivayo, na mkewe, Lucy “Lulu” Muteke, waliofariki dunia katika ajali ya helikopta, wanatarajiwa kuzikwa pamoja Alhamisi, Oktoba 8, 2026, katika makaburi ya Glen Forest jijini Harare, Zimbabwe.
Taarifa hiyo imetolewa na msemaji wa familia, Herbert Chivayo, aliyesema maandalizi ya mazishi yamekamilika baada ya kukamilishwa kwa taratibu za uchunguzi wa miili pamoja na mashauriano kati ya familia za wanandoa hao.
Chivayo na mkewe walifariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea eneo la karibu na Marondera, Zimbabwe, na kusababisha familia, ndugu na marafiki kuanza maandalizi ya kuwaaga.
Herbert alisema familia imeamua wanandoa hao wazikwe katika eneo moja, huku ikieleza kuwa hakutakuwa na utaratibu wa waombolezaji kuiona miili yao kabla ya mazishi kutokana na hali yake baada ya ajali.
Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia hali ya miili hiyo baada ya ajali, huku familia ikiendelea na maandalizi ya mwisho ya mazishi.
#ArushaDigitalUpdate
.....Ends.....

Post a Comment