Ad
Breaking🔥

UKRAINE YARUSHA DRONI ZAIDI YA 1,000 URUSI


UKRAINE YARUSHA DRONI ZAIDI YA 1,000 URUSI

By Arushadigital-MOSCOW, URUSI
UKRAINE imerusha zaidi ya droni 1,000 kuelekea maeneo mbalimbali nchini Urusi, huku mamia zikilenga Moscow, katika shambulio ambalo Meya wa mji huo, Sergei Sobyanin, amelieleza kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea dhidi ya mji huo.

Shambulio hilo limetokea wakati Urusi ikihitimisha siku ya tatu na ya mwisho ya uchaguzi wa bunge, huku mamlaka zikisema watu wawili wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika eneo la Moscow.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, shambulio hilo pia limesababisha uharibifu katika kiwanda cha kusafisha mafuta pamoja na 
jengo la makazi.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema Kyiv ilitumia droni pamoja na makombora yaliyotengenezwa nchini humo, yakiwamo aina za Flamingo na Pelican, kulenga vituo vya mafuta na miundombinu ya usafirishaji nchini Urusi.

Zelenskyy amesema mashambulizi hayo ni sehemu ya mkakati wa kuongeza shinikizo la kiuchumi kwa Urusi kwa kulenga miundombinu inayosaidia kugharamia vita vinavyoendelea kati ya nchi hizo.

Wakati huo huo, amesema Ukraine inaendelea kukabiliana na mashambulizi ya Urusi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuzuia na kuangusha jumla ya droni 1,110 za Ukraine katika maeneo mbalimbali ya Urusi, Crimea na Bahari Nyeusi.

Meya wa Moscow, Sobyanin, amesema takribani droni 450 ziliharibiwa kabla ya kufika katika mji huo, huku operesheni za ulinzi na usafishaji wa maeneo yaliyoathiriwa zikiendelea.

#ArushaDigital#


Post a Comment

Previous Post Next Post