LUKUMAY AMLILIA LEMA,ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO
Na Joseph Ngilisho | ARUSHA
Dkt. Lukumay amejijengea umaarufu kutokana na tabia yake ya kugusa katika makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo kutoa faraja bila kujali wadhifa alionao kwa kuwafikia watu wenye shida na kuwafariji.
LUKUMAY amefika nyumbani kwa marehemu Kaloleni, jijini Arusha, Septemba 26, 2026, kuungana na wananchi na viongozi mbalimbali kutoa pole na faraja kwa familia.
Dkt. Lema alifariki Septemba 23, 2026 katika Hospitali ya Selian (ALMC) jijini Arusha. Kwa mujibu wa taarifa ya msiba, marehemu alitumia kipindi cha uhai wake katika kuendeleza huduma ya SAFINA Redio, akiacha alama katika maisha ya waumini, wasikilizaji na watu mbalimbali walioguswa na huduma hiyo.
SAFINA Redio, iliyopo Kaloleni jijini Arusha, ilianzishwa na Dkt. Lema na imekuwa ikijikita katika huduma za kiroho na mawasiliano ya kidini.
Ends

إرسال تعليق