Breaking🔥

LISSU AENDELEA NA UTETEZI KESI YA UHAINI, AOMBA RAIS SAMIA AITWE KUTOA USHAHIDI

LISSU AENDELEA NA UTETEZI KESI YA UHAINI, AOMBA RAIS SAMIA AITWE KUTOA USHAHIDI

Na Joseph Ngilisho | DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, leo Agosti 24, 2026, ameendelea na utetezi wake katika kesi ya uhaini inayomkabili, inayosikilizwa katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Lissu, ambaye pia ni Wakili wa Mahakama Kuu, alianza kujitetea Agosti 21, mwaka huu, baada ya mahakama kuamua kuwa ana kesi ya kujibu.

Katika hatua zake za utetezi, Lissu ameendelea kuwasilisha hoja kuhusu mashahidi anaotaka waitwe kutoa ushahidi upande wake, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jopo la Majaji watatu, likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16, kama ilivyorekebishwa mwaka 2023.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akishikiliwa tangu Aprili 3, 2025, baada ya kukamatwa akihusishwa na tuhuma za kushawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kesi hiyo inaendelea leo huku hatua za utetezi wa Lissu zikifuatiliwa kwa karibu, hasa kuhusu maombi yake ya kuitwa kwa mashahidi mbalimbali wa upande wa utetezi na uamuzi wa mahakama juu ya maombi hayo.

Post a Comment

أحدث أقدم