Breaking🔥

JAMHURI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA UHAINI YA TUNDU LISSU,MASHAHIDI 13 WALIKUWA WAMEBAKI

JAMHURI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA UHaini YA TUNDU LISSU

Na Joseph Ngilisho | ArushaDigital

DAR ES SALAA: Upande wa Jamhuri umefunga rasmi ushahidi wake katika kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, baada ya kutangaza mahakamani kuwa mashahidi 17 waliowasilishwa katika kesi hiyo wametosheleza upande wa mashtaka licha ya kuwa na mashahidi 13 wakibakia.

Uamuzi huo umefikiwa leo Jumatatu, Agosti 17, 2026, baada ya shahidi wa 17 kumaliza kuhojiwa na Lissu, hatua iliyokuwa ikifungua uwezekano wa Jamhuri kuwasilisha shahidi mwingine ambaye angekuwa wa 18.

Hata hivyo, matarajio hayo hayakutimia baada ya Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, kuwasilisha mahakamani taarifa ya maombi ya upande wa Jamhuri ya kufunga ushahidi wake.

Kupitia maombi hayo, upande wa mashtaka ulieleza kuwa mashahidi 17 waliowasilishwa katika kesi hiyo wametosheleza kutoa ushahidi unaohitajika kwa upande wa Jamhuri, hivyo hakuna shahidi mwingine atakayeitwa.

Hatua hiyo inaashiria kukamilika kwa awamu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi hiyo, ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu kutokana na uzito wa mashtaka yanayomkabili Lissu.

Baada ya Jamhuri kufunga ushahidi wake, hatua inayofuata itategemea maelekezo na uamuzi wa Mahakama kuhusu mwenendo wa kesi hiyo, ikiwamo namna upande wa utetezi utakavyoendelea na kesi yake.

Lissu anakabiliwa na kesi ya Uhaini, huku mwenendo wake ukiendelea mbele ya mahakama chini ya uangalizi mkubwa wa wadau mbalimbali.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم