RUJOMBA ANG'OKA AUWSA ARUSHA,MSUYA ACHUKUA NAFASI YAKE


AUWSA ARUSHA YAPATA MKURUGENZI MPYA

Na Joseph Ngilisho|ARUSHA 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) imepata Mkurugenzi Mtendaji mpya, Mhandisi Iddy Yazid Msuya, kufuatia uhamisho wake wa kikazi kwenda mkoani Arusha.

Mhandisi Msuya anachukua nafasi ya Mhandisi Justine Rujomba ambaye amehamishiwa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuendelea na majukumu yake ya kikazi.

Mhandisi Rujomba

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Msuya alikuwa akihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA), ambako alisimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji safi na usafi wa mazingira.

Uhamisho huo ni sehemu ya mabadiliko ya kiutendaji yenye lengo la kuendelea kuimarisha usimamizi na utoaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira katika mamlaka mbalimbali nchini.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم