DKT LUKUMAY NA WAZIRI MCHENGERWA WATUA USWISI KWENYE MKUTANO MUHIMU WA AFYA (WHO)

 BY JOSEPH NGILISHO|Arushadigital

WAZIRI wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Johannes Lembulung Lukumay, wamepokea maelezo ya awali kutoka kwa Balozi Abdalah Saleh Possi kabla ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (World Health Organization) unaofanyika jijini Geneva, Uswisi, kuanzia Mei 17 hadi Mei 23, 2026.

Katika kikao hicho cha maandalizi, viongozi hao wamepatiwa taarifa muhimu kuhusu ajenda kuu za mkutano huo, ikiwemo masuala ya ustawi wa afya ya umma duniani, udhibiti na uzuiaji wa magonjwa ya mlipuko, pamoja na mikakati ya kuimarisha mifumo ya afya katika nchi mbalimbali.

Mkutano huo wa WHO unawakutanisha mawaziri wa afya, wataalamu na wadau wa sekta ya afya kutoka mataifa mbalimbali duniani, ukiwa jukwaa muhimu la kujadili changamoto na fursa za sekta ya afya kwa ngazi ya kimataifa.

Tanzania inashiriki kikamilifu katika mkutano huo kwa lengo la kuhakikisha inalinda na kuendeleza maslahi ya afya ya wananchi wake, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuboresha huduma za afya na kukabiliana na changamoto za kiafya duniani.

Ends

Post a Comment

0 Comments