MBUNGE DR. LUKUMAY AKETI MEZA MOJA NA RAIS SAMIA, AJADILI MASUALA YA AFYA
Na Joseph Ngilisho-Arushadigital| Dar es Salaam
Mkutano huo mkubwa wa kimataifa umewakutanisha wataalamu wa afya kutoka mataifa mbalimbali duniani, ukilenga kujadili maendeleo ya sayansi ya tiba, kubadilishana uzoefu pamoja na kuimarisha huduma za upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Miongoni mwa viongozi wa kitaifa waliopata fursa ya kushiriki katika mkutano huo ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt Johannes Lembulung Lukumay, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI. Dr. Lukumay alionekana akiwa katika meza moja na Rais Samia, hatua inayoashiria umuhimu wa ushirikiano kati ya mihimili ya dola katika kuimarisha sekta ya afya nchini.
.ends..

0 Comments