NKUSI AELEZA HATUA ZA UTEKELEZAJI MIRADI YA BIL.30 YA TACTIC PACKAGE 2 JIJI LA ARUSHA.

NKUSI AELEZA HATUA ZA UTEKELEZAJI MIRADI YA BIL.30 YA TACTIC PACKAGE 2 JIJI LA ARUSHA.

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA: 

MENEJA wa Mradi wa Tactic ,Evelyn Nkuzi, amesema utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na mkandarasi Mohamed Builders unaendelea vizuri huku thamani ya mkataba huo ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 30.


Nkuzi amesema mkataba huo mmoja unajumuisha miradi minne mikubwa ambayo ni mradi wa soko la Kilombero, mradi wa stendi ya mabasi Bondeni City (Package 2), mradi wa soko la Mrombo pamoja na mradi wa wachezaji.


Alieleza hayo wakati wa ziara ya  Waziri Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Mbunge wa jimbo la Arusha,Paul Makonda wakati alipotembelea miradi miwili kati ya Minne inayotekelezwa, ambayo ni Stendi ya mabasi Bondeni City pamoja na soko la Kilombero  .


Ramani ya Soko la Kilombero likikamilika .

Kwa mujibu wa  Nkuzi, mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Bondeni City umefikia asilimia 48 ya utekelezaji wake. Mradi huo ulianza rasmi tarehe 30 Mei 2025 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Mei 2026, huku gharama zake zikifikia takribani shilingi bilioni 14.


Kwa upande wa mradi wa soko la Kilombero, amesema nao ulianza tarehe 30 Mei 2025 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Mei 2026.


Alisema Mradi huo umefikia asilimia 64.7 ya utekelezaji wake, ikiwa ni hatua ya mwisho kuelekea ukamilishaji. Gharama za utekelezaji wa mradi huo ni shilingi bilioni 9.5.


Nkuzi aliwahakikishia viongozi na wananchi kuwa mkandarasi anaendelea na kazi kwa kasi na ubora unaotakiwa, bila kubadilisha usanifu wa miradi wala kuongeza gharama zisizokuwa kwenye mkataba, huku fedha za serikali zikitumika kwa uangalifu na uwajibikaji mkubwa.


Alisema lengo ni kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati ili kuleta tija kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo husika.




Ends..

Post a Comment

0 Comments