By Arushadigital-Dar Es Salaam
Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi la Chadema, katika kesi ya madai namba 8323/2025 inayohusu mgawanyo wa rasilimali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, iliyofunguliwa na Makamu mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Zanzibar Said Issa Mohamed, pamoja na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Wadaiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, ni Bodi ya Wadhamini Waliosajiliwa wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Wadai wanasema kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali za chama na rasilimali za kifedha kati ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara, kinyume cha Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya chama hicho.
Pia wanadai kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia, pamoja na utoaji wa maoni na matamko yenye nia ya kuvuruga Muungano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ends..

0 Comments